Methali 17:26-28 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Si vizuri kumtoza faini mtu asiye na hatia;ni kosa kumchapa viboko muungwana.

27. Asiyesema sana ana maarifa;mtu mtulivu ni mwenye busara.

28. Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima;akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili.

Methali 17