Methali 13:7-19 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Baadhi hujidai kuwa matajiri kumbe hawana kitu;wengine hujiona kuwa maskini hali wana mali tele.

8. Fidia ya mtu ni mali yake,lakini maskini hana cha kutishwa.

9. Mwadilifu hungaa kama taa iwakayo vizuri,lakini waovu ni kama taa inayozimika.

10. Kiburi husababisha tu ugomvi,lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima.

11. Mali ya harakaharaka hutoweka,lakini akusanyaye kidogokidogo ataiongeza.

12. Tumaini la kungojangoja huumiza moyo,lakini tazamio linalotimia ni mti wa uhai.

13. Anayedharau mawaidha anajiletea maangamizi,lakini anayetii amri atapewa tuzo.

14. Mafundisho ya wenye hekima ni chemchemi ya uhai;humwezesha mtu kuiepa mitego ya kifo.

15. Kuwa na akili huleta fadhili,lakini njia ya waovu ni ya taabu

16. Mwenye busara hutenda kila kitu kwa akili,lakini mpumbavu hutembeza upumbavu wake.

17. Mjumbe mbaya huwatumbukiza watu taabuni,lakini mjumbe mwaminifu huleta nafuu.

18. Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho,lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa.

19. Inafurahisha upatapo kile unachotaka,kwa hiyo wapumbavu huchukia kuepa uovu.

Methali 13