Methali 12:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Apendaye nidhamu hupenda maarifa,bali asiyependa kuonywa ni mjinga.

2. Mtu mwema hufadhiliwa na Mwenyezi-Mungu,lakini mwenye nia mbaya hulaaniwa na Mungu.

3. Mtu hawi imara kwa kutenda maovu,lakini hakuna kiwezacho kumngoa mtu mwadilifu.

4. Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe;amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake.

Methali 12