Methali 11:19-26 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Mtu anayepania kuwa mwadilifu ataishi,lakini anayechagua kutenda maovu atakufa.

20. Wenye nia mbaya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,lakini wenye mwenendo mwema ni furaha yake.

21. Hakika mwovu hataepa kuadhibiwa,lakini waadilifu wataokolewa.

22. Mwanamke mzuri asiye na akili,ni kama pete ya dhahabu puani mwa nguruwe.

23. Matazamio ya waadilifu yana matokeo mema;tamaa za waovu huishia katika ghadhabu.

24. Atoaye kwa ukarimu huzidi kutajirika;lakini bahili huzidi kudidimia katika umaskini.

25. Mtu mkarimu atafanikishwa,amnyweshaye mwingine maji naye atanyweshwa.

26. Watu humlaani afichaye nafaka,lakini humtakia baraka mwenye kuiuza.

Methali 11