Methali 11:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,lakini matumizi ya kipimo halali ni furaha kwake.

2. Kiburi huandamana na fedheha,lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima.

3. Unyofu wa watu wema huwaongoza,upotovu wa wenye hila huwaangamiza.

Methali 11