7. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa,lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
8. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,wala usiyapuuze mafundisho ya mama yako;
9. hayo yatakupamba kilemba kichwani pako,kama mkufu shingoni mwako.
10. Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi.
11. Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua;njoo tukawashambulie wasio na hatia!
12. Tutawameza kama Kuzimu wakiwa hai,watakuwa kama wale washukao Shimoni.