10. Ufalme wako ufike.Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
11. Utupe leo chakula chetu cha kila siku.
12. Utusamehe makosa yetu,kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
13. Usitutie katika majaribu,lakini utuokoe na yule Mwovu.’ [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
14. “Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi pia.
15. Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe nyinyi makosa yenu.
16. “Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni kweli, hao wamekwisha pata tuzo lao.
17. Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako,
18. ili mtu yeyote asijue kwamba unafunga, ila ujulikane tu kwa Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
19. “Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba.
20. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba.