Mathayo 4:18-22 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaye Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.

19. Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu.”

20. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

21. Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi, Yesu akawaita,

22. nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.

Mathayo 4