Mathayo 28:2-7 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Ghafla kukatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.

3. Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.

4. Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa kama wamekufa.

5. Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Nyinyi msiogope! Najua kwamba mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.

6. Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.

7. Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka kwa wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni.”

Mathayo 28