36. Huyo mtu akawatuma tena watumishi wengine, wengi kuliko wa safari ya kwanza. Wale wakulima wakawatendea namna ileile.
37. Mwishowe akamtuma mwanawe huku akifikiri: ‘Watamjali mwanangu.’
38. Lakini wale wakulima walipomwona mwanawe wakasemezana wao kwa wao: ‘Huyu ndiye mrithi; na tumuue ili tuuchukue urithi wake!’
39. Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua.
40. “Sasa, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyaje hao wakulima?”