Mathayo 18:27-32 Biblia Habari Njema (BHN)

27. Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake.

28. “Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha dinari 100. Akamkamata, akamkaba koo akisema, ‘Lipa deni lako!’

29. Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, ‘Unisubiri nami nitakulipa’.

30. Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni.

31. “Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.

32. Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote.

Mathayo 18