20. Yesu akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani, iwe ndogo hata kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu: ‘Toka hapa uende pale,’ nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho hakingewezekana kwenu. [
21. Pepo wa namna hii hawezi kuondolewa ila kwa sala na kufunga.”]
22. Walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu aliwaambia, “Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watu.
23. Watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunzi wakahuzunika mno.