8. Maana Mwana wa Mtu ana uwezo juu ya Sabato.”
9. Yesu alitoka hapo, akaenda katika sunagogi lao.
10. Kulikuwa na mtu mmoja mwenye mkono uliopooza. Basi, watu wakamwuliza Yesu, “Je, ni halali kumponya mtu siku ya Sabato?” Walimwuliza hivyo wapate kisa cha kumshtaki.