Mathayo 1:7-18 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Solomoni alimzaa Rehoboamu,Rehoboamu alimzaa Abiya,Abiya alimzaa Asa,

8. Asa alimzaa Yehoshafati,Yehoshafati alimzaa Yoramu,Yoramu alimzaa Uzia,

9. Uzia alimzaa Yothamu,Yothamu alimzaa Ahazi,Ahazi alimzaa Hezekia,

10. Hezekia alimzaa Manase,Manase alimzaa Amoni,Amoni alimzaa Yosia,

11. Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.Huo ulikuwa wakati Wayahudi walipopelekwa uhamishoni Babuloni.

12. Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishoni Babuloni,Yekonia alimzaa Shealtieli,Shealtieli alimzaa Zerubabeli,

13. Zerubabeli alimzaa Abiudi,Abiudi alimzaa Eliakimu,Eliakimu alimzaa Azori,

14. Azori alimzaa Zadoki,Zadoki alimzaa Akimu,Akimu alimzaa Eliudi,

15. Eliudi alimzaa Eleazari,Eleazari alimzaa Mathani,Mathani alimzaa Yakobo,

16. Yakobo alimzaa Yosefu, mumewe Maria mama yake Yesu aitwaye Kristo.

17. Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo.

18. Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke, alionekana kuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Mathayo 1