9. Chakula chetu twapata kwa kuhatarisha maisha yetu,maana wauaji wanazurura huko mashambani.
10. Ngozi zetu zawaka moto kama tanurikwa sababu ya njaa inayotuchoma.
11. Wanawake wetu wanashikwa kwa nguvu mjini Siyoni,binti zetu katika vijiji vya Yuda.
12. Wakuu wetu wametungikwa kwa mikono yao;wazee wetu hawapewi heshima yoyote.
13. Vijana wanalazimishwa kusaga nafaka kwa mawe,wavulana wanayumbayumba kwa mizigo ya kuni.
14. Wazee wameacha kutoa mashauri yao,vijana wameacha kuimba.