18. Maana mlima Siyoni umeachwa tupu,mbweha wanazurura humo.
19. Lakini wewe Mwenyezi-Mungu watawala milele,utawala wako wadumu vizazi vyote.
20. Mbona umetuacha muda mrefu hivyo?Mbona umetutupa siku nyingi hivyo?
21. Uturekebishe ee Mwenyezi-Mungu, nasi tukurudie,uturudishie fahari yetu kama zamani.
22. Au, je, umetukataa kabisa?Je, umetukasirikia mno?