Maombolezo 3:57-62 Biblia Habari Njema (BHN)

57. Nilipokuita ulinijia karibuukaniambia, ‘Usiogope!’

58. “Umenitetea katika kisa changu ee Mwenyezi-Mungu,umeyakomboa maisha yangu.

59. Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu,uniamulie kwa wema kisa changu.

60. Umeuona uovu wa maadui zangu,na mipango yao yote ya hila dhidi yangu.

61. “Umesikia matukano yao ee Mwenyezi-Mungu,na mipango yao yote ya hila dhidi yangu.

62. Maneno na mawazo ya maadui zangu siku nzimani juu ya kuniangamiza mimi.

Maombolezo 3