Maombolezo 3:52-58 Biblia Habari Njema (BHN)

52. “Nimewindwa kama ndegena hao wanichukiao bila sababu.

53. Walinitupa shimoni nikiwa haina juu yangu wakarundika mawe.

54. Maji yalianza kunifunika kichwa,nami nikafikiri, ‘Huu ni mwisho wangu.’

55. “Kutoka chini shimoninilikulilia ee Mwenyezi-Mungu.

56. Wewe umenisikia nikikulilia:‘Usiache kusikia kilio changu cha msaadabali unipatie nafuu.’

57. Nilipokuita ulinijia karibuukaniambia, ‘Usiogope!’

58. “Umenitetea katika kisa changu ee Mwenyezi-Mungu,umeyakomboa maisha yangu.

Maombolezo 3