Maombolezo 3:5-10 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Amenizingira na kunizungushiauchungu na mateso.

6. Amenikalisha gizanikama watu waliokufa zamani.

7. Amenizungushia ukuta nisitoroke,amenifunga kwa minyororo mizito.

8. Ingawa naita na kulilia msaadaanaizuia sala yangu isimfikie.

9. Njia zangu ameziziba kwa mawe makubwaamevipotosha vichochoro vyangu.

10. Yeye ni kama dubu anayenivizia;ni kama simba aliyejificha.

Maombolezo 3