10. Wazee wa Siyoni wameketi chini kimya,wamejitia mavumbi vichwanina kuvaa mavazi ya gunia.Wasichana wa Yerusalemu wameinamisha vichwa.
11. Macho yangu yamevimba kwa kulia,roho yangu imechafuka.Moyo wangu una huzuni nyingikwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangukwa sababu watoto wachanga wanazirai katika barabara za mji.
12. Wanawalilia mama zao:“Wapi chakula, wapi kinywaji?”Huku wanazirai kama majeruhikatika barabara za mjini,na kukata roho mikononi mwa mama zao.
13. Nikuambie nini ee Yerusalemu?Nikulinganishe na nini?Nikufananishe na kitu ganiili niweze kukufariji,ee Siyoni uliye mzuri?Maafa yako ni mengi kama bahari.Ni nani awezaye kukuponya?