Malaki 4:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Siku hiyo mtawakanyagakanyaga waovu, nao watakuwa kama majivu chini ya nyayo zenu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.

4. “Kumbukeni sheria, kanuni na maagizo yangu niliyomwamuru Mose mtumishi wangu kule mlimani Horebu, ili awaamuru watu wote wa Israeli.

5. “Tazama, kabla ya kufika siku ile kuu na ya kutisha, nitamtuma nabii Elia.

6. Nabii Elia atawapatanisha wazazi na watoto wao; la sivyo, nitakuja na kuiangamiza nchi yenu.”

Malaki 4