Luka 19:43-47 Biblia Habari Njema (BHN)

43. Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote.

44. Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako ndani ya kuta zako; hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu hukuutambua wakati Mungu alipokujia kukuokoa.”

45. Kisha, Yesu aliingia hekaluni, akaanza kuwafukuza nje wafanyabiashara

46. akisema, “Imeandikwa: ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala’; lakini nyinyi mmeifanya kuwa pango la wanyanganyi.”

47. Yesu akawa anafundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu, waalimu wa sheria na viongozi wa watu walitaka kumwangamiza,

Luka 19