Kutoka 8:30-32 Biblia Habari Njema (BHN)

30. Basi, Mose akaondoka nyumbani kwa Farao, akamwomba Mwenyezi-Mungu.

31. Mwenyezi-Mungu akafanya kama Mose alivyomwomba, wale nzi wakatoweka kutoka kwa Farao, maofisa wake na watu wake, wala hakusalia hata mmoja.

32. Lakini hata safari hii Farao alikuwa mkaidi, wala hakuwaruhusu Waisraeli kuondoka.

Kutoka 8