18. Matawi sita yalitokeza kila upande wa ufito wake, matawi matatu upande mmoja na matawi matatu upande mwingine.
19. Katika kila tawi kulikuwa na vikombe vitatu mfano wa maua ya mlozi, kila kimoja na tumba lake na ua lake.
20. Na katika ufito kulikuwa na vikombe vinne mfano wa maua ya mlozi, pamoja na matumba yake na maua yake.
21. Mahali pale palipotokezea jozi tatu za matawi chini ya kila jozi kulikuwa na tumba moja.
22. Matumba hayo na matawi vilikuwa kitu kimoja na kinara hicho, na chote kilifuliwa kwa dhahabu safi.
23. Alikitengenezea taa saba, koleo na visahani vyake kwa dhahabu safi.
24. Alikitengeneza kinara hicho na vifaa vyake kwa kilo thelathini na tano za dhahabu.