14. na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba. Utaifunga mikufu hiyo kwenye hivyo vijalizo.
15. “Utatengeneza kifuko cha kifuani cha kauli cha maamuzi; kitengenezwe kwa ustadi sawa kama kilivyotengenezwa kile kizibao: Kwa dhahabu, kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa.
16. Kifuko hicho ambacho kimekunjwa kitakuwa cha mraba, sentimita 22.
17. Kitapambwa kwa safu nne za mawe ya thamani: Safu ya kwanza itakuwa ya akiki, topazi na almasi nyekundu;
18. safu ya pili itakuwa ya zumaridi, johari ya rangi ya samawati na almasi;
19. safu ya tatu itakuwa ya yasintho, akiki nyekundu na amethisto;
20. na safu ya nne itakuwa ya zabarajadi, shohamu na yaspi; yote yatatiwa kwenye vijalizo vya dhahabu.