Kutoka 25:24-29 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Hiyo meza utaipaka dhahabu safi na kuizungushia utepe wa dhahabu.

25. Kisha utaizungushia ubao wenye upana wa sentimita 66.

26. Utaitengenezea pete nne za dhahabu na kuzitia kwenye pembe zake miguuni pake.

27. Pete hizo zitakuwa karibu na ule ubao wa kuizunguka meza na zitakuwa za kushikilia mipiko ya kuibebea hiyo meza.

28. Utatengeneza mipiko ya mjohoro na kuipaka dhahabu; mipiko itakuwa ya kuibebea hiyo meza.

29. Utatengeneza sahani na vikombe vya kuwekea ubani mezani, na pia bilauri na bakuli za kumiminia tambiko za kinywaji. Vifanye vyombo hivyo vyote kwa dhahabu safi.

Kutoka 25