4. “Magari na majeshi ya Farao ameyatumbukiza baharini,maofisa wake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
5. Vilindi vya maji vimewafunika,wameporomoka baharini kama jiwe.
6. “Mkono wako wa kulia ee Mwenyezi-Mungu watukuka kwa nguvu;kwa mkono wako wa kulia ee Mwenyezi-Mungu wawaponda adui.
7. Kwa wingi wa ukuu wako wawaangamiza wapinzani wako;wawapulizia ghadhabu yako nayo yawateketeza kama makapi.
8. Kwa pumzi ya pua yako maji yalirundikana,mawimbi yakasimama wima kama ukuta;vilindi katikati ya bahari vikagandamana.
9. Adui alijisemea, ‘Nitawafuata na kuwakamata;nitagawanya nyara mpaka hamu yangu iishe.Tutaufuta upanga wetu,tutawaangamiza kwa mkono wetu.’
10. Lakini wewe uliuvumisha upepo wako,nayo bahari ikawafunika.Walizama majini kama risasi.
11. “Ewe Mwenyezi-Mungu,ni nani kati ya miungu anayelingana nawe?Ni nani aliye kama wewe uliye mtakatifu mkuu,utishaye kwa matendo matukufu,unayetenda mambo ya ajabu?