Kumbukumbu La Sheria 33:15-18 Biblia Habari Njema (BHN)

15. kwa mazao bora ya milima ya kale,na mazao tele ya milima ya kale,

16. Nchi yake ijae yote yaliyo mema,ibarikiwe kwa wema wa Mwenyezi-Mungu,ambaye alitokea katika kichaka.Baraka hizi ziwashukie watu wa kabila la Yosefu,aliyekuwa mkuu miongoni mwa ndugu zake.

17. Fahari yake ni fahari ya fahali wa kwanza,pembe zake ni za nyati dume.Atazitumia kuyasukuma mataifa;yote atayasukuma mpaka miisho ya dunia.Efraimu atakuwa na pembe hizo 10,000na Manase kwa maelfu.”

18. Juu ya kabila la Zebuluni na kabila la Isakari, alisema,“Zebuluni, furahi katika safari zako;nawe Isakari, furahi katika mahema yako.

Kumbukumbu La Sheria 33