Kumbukumbu La Sheria 32:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Tegeni masikio enyi mbingu:Sikiliza, ee dunia, maneno ninayosema.

2. Mafundisho yangu na yatone kama mvua,maneno yangu yadondoke kama umande,kama manyunyu kwenye mimea michanga,kama mvua nyepesi katika majani mabichi.

3. Maana nitalitangaza jina la Mwenyezi-Mungu,nanyi mseme, ‘Mungu wetu ni Mkuu’.

Kumbukumbu La Sheria 32