Kumbukumbu La Sheria 28:5-8 Biblia Habari Njema (BHN)

5. “Vikapu vyenu vya nafaka vitabarikiwa na vyombo vyenu vya kukandia.

6. Mtabarikiwa mnaporudi nyumbani na mnapotoka nje.

7. Maadui zenu wakiwashambulia, Bwana atawapeni ushindi juu yao. Wakija kuwashambulia kwa njia moja watawakimbieni kwa njia saba.

8. Baraka za Mwenyezi-Mungu zitakuwa katika ghala zenu za nafaka na katika shughuli zenu zote. Atawabariki katika nchi ambayo anawapeni.

Kumbukumbu La Sheria 28