Kumbukumbu La Sheria 23:12-15 Biblia Habari Njema (BHN)

12. “Lazima muwe na mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda haja.

13. Kati ya vifaa vyenu mtakuwa na jembe, na hilo mtatumia kuchimba shimo na kufukia kinyesi chenu.

14. Kambi yenu lazima iwe takatifu kwa kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anatembea kambini mwenu ili awaokoe na kuwatia adui zenu mikononi mwenu. Kwa hiyo msimwache aone kitu chochote kisichofaa miongoni mwenu, la sivyo atawaacheni.

15. “Mtumwa akikimbilia kwako usimrudishe kwa bwana wake.

Kumbukumbu La Sheria 23