Kumbukumbu La Sheria 20:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Kuna mwanamume yeyote hapa aliyeposa na yuko karibu kuoa? Arudi nyumbani, asije akafia vitani, na mwanamume mwingine akaoa mchumba wake.’

8. Maofisa wataendelea kuwaambia watu, ‘Je, yupo hapa mtu aliyekufa moyo? Arudi nyumbani, asije akasababisha wenzake kufa moyo kama yeye.’

9. Maofisa wakisha sema na watu, basi makamanda watawaongoza watu.

10. “Mnapokaribia mji kuushambulia, kwanza wapeni wakazi wake masharti ya amani.

11. Wakazi wa mji huo wakitaka amani na kujisalimisha kwenu, basi watu wote waliomo humo watawatumikieni na kufanya kazi za kulazimishwa.

12. Lakini wakazi wa mji huo wasipofanya amani nanyi, lakini wakapigana vita nanyi, basi, mtauzingira mji wao;

13. naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu akiutia mikononi mwenu, mtawaua kwa upanga wanaume wote;

Kumbukumbu La Sheria 20