Kumbukumbu La Sheria 19:16-19 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Ikiwa shahidi mdhalimu atatokea kumshtaki mtu yeyote juu ya kosa fulani,

17. basi yeye na mshtakiwa kuhusu mzozo huo watakwenda mbele ya Mwenyezi-Mungu, mbele ya makuhani na waamuzi ambao wako katika ofisi wakati huo;

18. waamuzi watachungua kwa uangalifu kesi hiyo na ikiwa mshahidi ni mshahidi wa uongo na amemshtaki mwenzake kwa uongo,

19. basi, mtamtendea alivyokusudia kumtendea ndugu yake. Ndivyo mtakavyokomesha uovu kati yenu.

Kumbukumbu La Sheria 19