Kumbukumbu La Sheria 15:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Kila mwisho wa mwaka wa saba mtawasamehe wadeni wenu wote.

2. Hivi ndivyo mtakavyofanya: Kila mmoja aliyemkopesha jirani yake, alifute hilo deni, wala asijaribu kumdai kwa sababu Mwenyezi-Mungu mwenyewe ameamua deni hilo lifutwe.

3. Mnaweza kuwadai wageni, lakini madeni yote ya ndugu zenu wenyewe mtayafuta.

4. “Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki katika nchi anayowapa iwe mali yenu. Hakuna hata mmoja atakayekuwa maskini kati yenu,

5. mradi tu mumtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa kufuata kwa uangalifu amri ninazowapeni hivi leo.

6. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawabariki kama vile alivyowaahidi. Nanyi mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa. Kadhalika mtatawala mataifa mengi, lakini mataifa hayo hayatawatawala nyinyi.

Kumbukumbu La Sheria 15