Kumbukumbu La Sheria 14:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Mnaweza kula wanyama wafuatao: Ng'ombe, kondoo, mbuzi,

5. kulungu, paa, kongoni, mbuzimwitu, paa mweupe, pofu na mbuzi wa mlimani;

6. na kila mnyama mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na mwenye kucheua, huyo mnaweza kula.

7. Lakini msile mnyama yeyote ambaye kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili na hacheui; msile ngamia, sungura na pelele, ingawa hucheua lakini kwato zao hazikugawanyika sehemu mbili; hao ni najisi kwenu.

8. Pia msile nguruwe, maana ijapokuwa kwato zake zimegawanyika sehemu mbili, yeye hacheui; hao ni najisi kwenu, msile nyama zao wala msiguse mizoga yao.

9. “Mnaweza kula kila aina ya samaki wenye mapezi na magamba.

Kumbukumbu La Sheria 14