Hawatajenga nyumba zikaliwe na watu wengine,wala kulima chakula kiliwe na watu wengine.Maana watu wangu niliowachaguawataishi maisha marefu kama miti;wateule wangu watafurahia matunda ya jasho lao.