Isaya 65:2-7 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Mchana kutwa niliwanyoshea mikono watu waasi,watu ambao hufuata njia zisizo sawa,watu ambao hufuata fikira zao wenyewe.

3. Ni watu ambao daima hunichokoza waziwazi;hutambikia miungu yao katika bustani,na kuifukizia ubani juu ya matofali.

4. Huketi makaburini na kukaa mafichoni usiku.Hula nyama ya nguruwe na mchuzi wa wanyama haramu.

5. Huwaambia wale wanaokutana nao:‘Kaeni mbali nami;msinikaribie kwani mimi ni mtakatifu!’Watu hao wananikasirisha mno,hasira yangu ni kama moto usiozimika.

6. “Jueni kuwa nimelitia jambo hilo moyoni,sitanyamaza bali nitawafanya walipe;nitawafanya walipe kwa wingi.

7. Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yaowayalipie na maovu ya wazee wao.Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani,wakanitukana mimi huko vilimani.Nitawafanya walipe kwa wingi,watayalipia matendo yao ya awali.”

Isaya 65