Isaya 65:14-17 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Watumishi wangu wataimba kwa furaha moyoni,lakini nyinyi mtalia kwa uchungu moyonina kupiga kelele kwa uchungu mkubwa rohoni.

15. Wale niliowachagua nitawapa jina jipya.Lakini nyinyi jina lenu watalitumia kulaania;‘Watasema: Bwana Mungu awaue kama hao.’

16. Basi, mwenye kujitakia baraka nchini,atajitakia baraka kwa Mungu wa kweli.Mwenye kuapa katika nchi hii,ataapa kwa Mungu wa kweli.Maana taabu za zamani zimepitazimetoweka kabisa mbele yangu.

17. “Sasa, naumba mbingu mpya na dunia mpya.mambo ya zamani hayatakumbukwa tena.

Isaya 65