Isaya 62:6-10 Biblia Habari Njema (BHN)

6. “Juu ya kuta zako ee Yerusalemu nimeweka walinzi,usiku na mchana kamwe hawatakaa kimya.”Enyi mnaomkumbusha Mwenyezi-Mungu ahadi yake,msikae kimya;

7. msimpe hata nafasi ya kupumzika,mpaka atakapousimika mji wa Yerusalemu,na kuufanya uwe fahari ulimwenguni kote.

8. Mwenyezi-Mungu ameapa kwa mkono wake wa kulia,naam, ameapa kwa mkono wake wenye nguvu akisema:“Sitawapa tena maadui zako nafaka yako;wala wageni hawatakunywa tena divai yakoambayo umeitolea jasho.

9. Bali nyinyi mliyoivuna nafaka hiyo,mtaila na kunitukuza mimi Mwenyezi-Mungu.Nyinyi mliochuma zabibu hizo,mtakunywa divai yake katika nyua zangu takatifu.”

10. Wakazi wa Yerusalemu, tokeni, tokeni nje ya mji,watayarishieni njia watu wenu wanaorejea!Jengeni! Jengeni barabara na kuondoa mawe yote!Wekeni alama kwa ajili ya watu.

Isaya 62