Isaya 61:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Watayajenga upya magofu ya zamani,wataisimika miji iliyoharibiwa hapo kwanza;wataitengeneza miji iliyobomolewa,uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita.

5. Wageni watakuwa hapo kuwachungia mifugo yenu;watawalimia na kuwatunzia mizabibu yenu.

6. Nanyi mtaitwa: “Makuhani wa Mwenyezi-Mungu”,Mtaitwa: “Watumishi wake Mungu wetu”.Mtafaidika kwa utajiri wa mataifa,mtatukuka kwa mali zao.

7. Kwa vile mlipata aibu maradufu,watu wakaona kuwa fedheha ni majaliwa yenu,sasa mtapata eneo maradufu kuwa mali yenu,na furaha yenu itadumu milele.

Isaya 61