13. Kwa hiyo, watu wangu watapelekwa uhamishonikwa sababu ya utovu wao wa akili.Watu wenu mashuhuri watakufa njaa,watu wengi watakufa kwa kiu.
14. Kuzimu inawangoja kwa hamu kubwa,imepanua kinywa chake mpaka mwisho.Waheshimiwa pamoja na raia wa Yerusalemuwanaingia humo makundi kwa makundi,kadhalika na wote wanaousherehekea.
15. Kila mtu atafedheheshwa,na wenye kiburi wote wataaibishwa.