20. Sasa, ondokeni Babuloni!Kimbieni kutoka Kaldayo!Tangazeni jambo hili kwa sauti za shangwe,enezeni habari zake kila mahali duniani.Semeni: “Mwenyezi-Mungu amelikomboataifa la mtumishi wake Yakobo.”
21. Alipowaongoza jangwani hawakuona kiu,aliwatiririshia maji kutoka mwambani,aliupasua mwamba maji yakabubujika.
22. Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu waovu sitawapa amani.”