Isaya 45:22-25 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Nigeukieni mimi mpate kuokolewa,popote mlipo duniani.Maana mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine.

23. Mimi nimeapa kwa nafsi yangu,ninachotamka ni ukweli,neno langu halitarudi nyuma:Kila binadamu atanipigia magoti,kila mtu ataapa uaminifu.

24. “Watasema juu yangu,‘Haki na nguvu viko kwa Mwenyezi-Mungu peke yake.’”Wote waliomwakia hasira Mwenyezi-Munguwatamjia yeye na kuaibishwa.

25. Lakini wazawa wa Israeliwatapata ushindi kwake Mwenyezi-Mungu na kufurahi.

Isaya 45