18. Mwenyezi-Mungu, Mungu pekee,ndiye aliyeiumba dunia,ndiye aliyeiumba na kuitegemeza.Hakuiumba iwe ghasia na tupu,ila aliiumba ikaliwe na viumbe vyake.Yeye asema sasa:“Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu,wala hakuna mwingine.
19. Mimi sikunena kwa siri,wala katika nchi yenye giza.Mimi sikuwaambia wazawa wa Yakobowanitafute katika ghasia.Mimi Mwenyezi-Mungu husema ukweli,maneno yangu ni ya kuaminika.”
20. Enyi watu wa mataifa mliosalia,kusanyikeni pamoja mje!Nyinyi mmekosa akili:Nyinyi mwabeba sanamu za mitina kumwomba mungu asiyeweza kuokoa watu.
21. Semeni wazi na kutoa hoja zenu;shaurianeni pamoja!Ni nani aliyetangaza zamani matukio ya sasa?Ni nani aliyetamka mambo haya zamani?Je, haikuwa mimi Mwenyezi-Mungu?Hakuna Mungu mwingine ila mimi!Mimi ni Mungu wa haki na mwokozi;hakuna mwingine ila mimi.
22. Nigeukieni mimi mpate kuokolewa,popote mlipo duniani.Maana mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine.