Isaya 43:15-19 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wenu;Mimi ndimi Muumba wa Israeli, Mfalme wenu.”

16. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wakati mmoja nilifanya barabara baharininikaweka njia kati ya mawimbi makubwa.

17. Nililipiga jeshi lenye nguvu,jeshi la magari na farasi wa vita,askari na mashujaa wa vita.Niliwaangusha chini wasiweze kuinuka tena,niliwakomesha na kuwazima kama utambi wa taa.Sasa nasema:

18. ‘Msiyanganganie mambo yaliyopita,wala msifikirie vitu vya zamani.

19. Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya.Kinafanyika sasa hivi,nanyi mtaweza kukiona.Nitafanya njia nyikani,na kububujisha mito jangwani.

Isaya 43