Isaya 42:11-19 Biblia Habari Njema (BHN)

11. jangwa na miji yake yote ipaaze sauti,vijiji vya wakazi wa Kedari vimsifu,wakazi wa Sela waimbe kwa shangwe;wapaaze sauti kutoka mlimani juu.

12. Wote wakaao nchi za mbali,na wamtukuze na kumsifu Mwenyezi-Mungu.

13. Mwenyezi-Mungu ajitokeza kama shujaa;kama askari vitani ajikakamua kupigana.Anapaza sauti kubwa ya vita,na kujionesha mwenye nguvu dhidi ya maadui zake.

14. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza,nimekaa kimya na kujizuia;lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua,anayetweta pamoja na kuhema.

15. Nitaharibu milima na vilima,na majani yote nitayakausha.Mito ya maji nitaigeuza kuwa nchi kavu,na mabwawa ya maji nitayakausha.

16. “Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu,nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui.Mbele yao giza nitaligeuza kuwa mwanga,na mahali pa kuparuza patakuwa laini.Huo ndio mpango wangu wa kufanya,nami nitautekeleza.

17. Wote wanaotegemea sanamu za miungu,wote wanaoziambia: Nyinyi ni miungu yetu;watakomeshwa na kuaibishwa.

18. “Sikilizeni enyi viziwi!Tazameni enyi vipofu, mpate kuona!

19. Nani aliye kipofu ila mtumishi wangu?Nani aliye kiziwi kama mjumbe ninayemtuma?Ni nani aliye kipofu kama huyu niliyemweka wakfu,au kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi-Mungu?

Isaya 42