Isaya 38:3-10 Biblia Habari Njema (BHN)

3. akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, nakusihi ukumbuke jinsi nilivyokutumikia kwa uaminifu na kwa moyo wangu wote, na kutenda yaliyo sawa mbele yako.” Hezekia akalia kwa uchungu sana.

4. Kisha neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Isaya:

5. “Nenda ukamwambie Hezekia, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa baba yako Daudi, anasema hivi: Nimesikia ombi lako na nimeyaona machozi yako. Basi, nakuongezea miaka kumi na mitano ya kuishi.

6. Nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mikononi mwa mfalme wa Ashuru na kuulinda.”

7. Isaya akamjibu, “Hii itakuwa ishara kwako kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwamba Mwenyezi-Mungu atafanya kama alivyoahidi.

8. Nitafanya kivuli kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi, kirudi nyuma hatua kumi.” Nacho kivuli kikarudi nyuma hatua kumi.

9. Kisha mfalme Hezekia alipopona, akatunga wimbo huu wa shukrani:

10. “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa,inanibidi niage dunia.Mimi nimepangiwa kwenda kuzimusiku zote zilizonibakia.

Isaya 38