Isaya 33:13-19 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Sikilizeni mambo mliyofanya enyi mlio mbali,nanyi mlio karibu kirini uwezo wangu.”

14. Wenye dhambi katika Siyoni wanaogopa,wasiomcha Mungu wanatetemeka na kusema:“Nani awezaye kuukaribia moto huu mkali?Nani awezaye kustahimili miali ya moto wa milele?”

15. Ni mtu aishiye kwa uadilifu na asemaye ukweli;mtu anayedharau kabisa utajiri wa dhuluma,anayekataa hongo kata kata,asiyekubali kamwe kusikia mipango ya mauaji,wala hakubali macho yake yaone maovu.

16. Mtu wa namna hiyo anaishi juu,mahali salama penye ngome na miamba;chakula chake atapewa daima,na maji yake ya kunywa hayatakosekana.

17. Mtaweza kumwona mfalme katika fahari yake,mtaiona nchi anayotawala, kubwa na pana.

18. Mtafikiria tisho lililopita na kujiuliza,“Wako wapi wale waliokadiria na kukisia kodi?Wako wapi wale waliopeleleza ulinzi wetu?”

19. Hamtawaona tena watu wale wenye kiburi,wanaozungumza lugha isiyoeleweka.

Isaya 33