1. Ole wako ewe mwangamizi,unayeangamiza bila wewe kuangamizwa!Ole wako wewe mtenda hila,ambaye hakuna aliyekutendea hila!Utakapokwisha kuangamizawewe utaangamizwa!Utakapomaliza kuwatendea watu hilawewe utatendewa hila.
2. Ee Mwenyezi-Mungu, utuonee huruma,kwako tumeliweka tumaini letu.Uwe kinga yetu kila siku,wokovu wetu wakati wa taabu.
3. Kwa kishindo cha sauti yako watu hukimbia;unapoinuka tu, mataifa hutawanyika.
4. Maadui zao wanakusanya mateka,wanayarukia kama panzi.