1. Ole wao wale waendao Misri kuomba msaada,ole wao wanaotegemea farasi,wanaotegemea wingi wa magari yao ya vita,na nguvu za askari wao wapandafarasi,nao hawamtegemei Mtakatifu wa Israeli,wala hawamwombi Mwenyezi-Mungu shauri!
2. Mungu ni mwenye busara na huleta maangamizi.Habadilishi tamko lake;ila yuko tayari kuwakabili watu waovukadhalika na wasaidizi wa watendao mabaya.
3. Wamisri ni binadamu tu wala si Mungu;farasi wao nao ni wanyama tu, si roho.Mwenyezi-Mungu akiunyosha mkono wake,taifa linalotoa msaada litajikwaa,na lile linalosaidiwa litaanguka;yote mawili yataangamia pamoja.